News

Posted On:: Dec, 05 2022
News Images

Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo TaSUBa usiku wa tarehe 4 Desemba 2022 wamekuwa kivutio kikubwa kwa wanavyuo wenzao waliohudhuria Hafla ya Utoaji Tuzo kwa wanavyuo inayojulikana kama UNI AWARDS 2022.

Wanafunzi hao kutoka chuo cha TaSUBa walikuwa kivutio kutokana na namna yao ya kuonesha furaha (vibe) wakati wote wa shuguli hiyo na pia furaha yao ilionekana kuzidi kwani waliweza kuondoka na tuzo takribani 4 kutoka vipengele tofauti tofauti.

Waliweza kuchukua kipengele cha mchoraji bora, muimbaji bora wa muziki wa injili, muigizaji bora na muimbaji bora wa kiume wa bongo fleva. Hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es salaam.

Chuo hicho kipo chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.