News

Posted On:: Sep, 26 2022
News Images

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa pongezi kwaBondiaMtanzania Twaha Kidukukwa kumchapa kwa alamaza majaji wote watatu (unanimous decision)BondiaAbdo Khaled kutokaMisri.

Kwa ushindi huo, bondia Kiduku amewezakuteteaubingwa wake waUBO Afrika (UBO all Africa Champion)na Mkanda mpya wa ubingwa wa Mabara(UBO Intercontinental).

Hili ni pambano la 20 kushindakwa Kiduku , akitokasare 1 na kupoteza8 akiwa na rekodi ya kuchezamapambano 29.

Mhe. Mchengerwa amefafanua kwamba dhamira ya Serikalikwa sasa ni kutumia michezo kuitangaza Tanzania.

Aidha, ametoa wito kwa wanamichezo kuthamini michezo na kufanya kama kazi inayoweza kubadili maisha yao na kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla.

Amesema, Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan itaendelea kusaidia wanamichezo wanaofanya vizuri ili wafike mbali.

Kwa upande wake muandaaji wa pambanohilo Selemani Semunyuameishukuru Serikali ya Awamuya Sitachini ya Rais Samia kwa mchango mkubwa wa uwekezajiinayofanyakwenye sekta za michezo na sanaa.

Amesema wao kama wadau wataendelea kuoneshavipaji walivyonavyo vijana na kuomba wadhamini kujitokeza kusaidia maandalizi, kwani kwa kutegemea viingilio pekee ni ngumu kukidhi gharama.

"Na Sasa dhamira yetu ni kufanya pambano kubwa Dar es Salaam au mkoa ambao unaweza kusaidia katika kutafuta udhamini wa pambano hilo" amefafanua Semunyu.

Pambano hilo lilipambwa na mapambano ya utangulizi ambayo yalikuwa na mvuto mkubwa kwa wadau hususan pambanobaina ya Emmilian Polino(JKT) na Osama Arabi (Mtwara) baada yabondia chipukizi Osamakuoneshakiwangokikubwahadi mwisho wa mchezo lichaya kushindwa katika pambano hilo.