News

Posted On:: Feb, 26 2024
News Images

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kuzifanya mbio za “Kili Marathon” kuwa bora zaidi duniani kutokana na ubora ulioonekana kuoneshwa na wakimbiaji wa mbio hizo katika bara Afrika kupitia Tanzania.

Hayo yamesemwa Februari 25, 2024 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro aliposhiriki mbio hizo za msimu wa 22 Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amewapongeza waandaji wa mbio hizo kwa kuzifanya kuwa za Afrika.

Mhe. Ndumbaro amesema kuwa, azma ya kuzipeleka mbio hizo duniani inawezekana kutokana na uwepo wa vivutio vingi vya utalii ambavyo vinavuta watu wengi kuja nchini.

Aidha Mhe. Ndumbaro amezitangaza mbio hizo kuwa, kuanzia sasa zitakua ni mbio mama kwa mbio zote nchini kutokana na kusababisha kuwepo kwa mbio nyingine nyingi zinazofanyika nchini.

Mbio za Kili Marathon mwaka huu zimehusisha wakimbiaji kutoka nchi 56 duniani ikiwemo Marekani, Uingereza, Uholanzi, Ufaransa Kenya, Uganda na Afrika Kusini kwa wakimbiaji wa umbali wa KM 42, KM 21, na KM 5.