Majukumu ya Wizara

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ina Majukumu yafuatayo:

  1. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sera za Sekta ya Utamaduni,Sanaa na Michezo.
  2. Kuendeleza, kuwezesha na kuratibu masuala ya kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara.
  3. Kusimamia na kuratibu Maendeleo ya Michezo nchini.
  4. Kusimamia na kuratibu Maendeleo ya Utamaduni nchini.
  5. Kusimamia utendaji wa Taasisi, Mashirika ya Umma, Wakala, Miradi na programu zilizo chini ya Wizara.