Mhe. Prof. Palamagamba J.A.M. Kabudi (Mb), Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa niaba ya nchi ya Tanzania na Mhe. Ongwang Peter kwa niaba ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya 4 (AUSC Region 4) wakisaini mkataba wa makubaliano ya nchi mwenyeji (Host Country Agreement) ili Tanzania kuwa makao makuu ya Sektretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika kanda ya 4.
Naibu Katibu Mkuu, Ndg. Methusela Ntonda akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa utamaduni mara baada ya kufungua kikao cha wadau wa utamaduni wanaoshiriki kuandaa orodha ya Kitaifa ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika, leo Agosti 19, 2025, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni hatua ya kukamilisha mchakato wa Uteuzi wa Muziki wa Singeli kwenye orodha ya kimataifa ya UNESCO.
Wataalamu wa Sekta ya Michezo katika Umoja wa Afrika Kanda ya 4, wakiwa katika siku ya pili ya mkutano wa pili wa kanda hiyo ngazi ya wataalamu, wenye lengo la kujadili maendeleo ya michezo katika ukanda huo leo Agosti 19, 2025, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akifungua Mafunzo ya Waandishi wa Habari na Utangazaji Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 leo tarehe 18 Agosti 2025 katika Ukumbi wa City Garden, jijini Mbeya.
Mhe. Hamis Mwinjuma (MB), Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Ndg. Gerson Msigwa, Katibu Mkuu wa Wizara wakishangilia ushindi wa Taifa Stars baada ya kuifungunga timu ya Madagascar kipigo cha Goli 2 - 1.
Sherehe za ufunguzi rasmi wa michuano ya CHAN 2024, leo Agosti 02, 2025, ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inachuana na Burkina Faso, katika Dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Mchezaji Mohamed Hussein akishangilia goli pamoja na wachezaji wenzake mara baada ya kufunga goli la pili dakika ya 74 hatimaye Tanzania kuibuka kidedea kwa kuipiga Burkina Faso kipigo cha Goli 2 - 0, yakiwa ni magoli ya kwanza katika michuano hiyo. (Goli la kwanza lilifungwa na Abdallah Sopu)
Uwanja wa Amaan Zanzibar ni moja ya viwanja vitavyotumika kwa ajili ya mechi za CHAN 2024 ambapo mechi zote za kundi D zitafanyika hapo.
Mh. Hamis Mwinjuma (MB), Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo azindua duka Mtandao la jezi za timu ya Taifa na kampeni ya "UTAIFA CHALLENGE"
Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa Mechi ya Ufunguzi ya CHAN 2024 tarehe 02 Agosti 2025.