Departments
Idara ya Maendeleo ya Utamaduni
Idara hii inasimamia na kuratibu shughuli zinazohusu utamaduni wa taifa letu. Katika kutekeleza majukumu yake, Idara imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni
- Sehemu ya Urithi na Utamaduni
- Sehemu ya Lugha
- Sehemu ya Maadili ya Taifa
Majukumu ya Idara hii ni pamoja na;
• Kuimarisha na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania ambao ni utambulisho wa taifa letu.
• Kuhimiza na kukuza utaifa kwa vijana wetu na wananchi kwa ujumla.
• Kukuza lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya Taifa .
• Kufanya tafiti za lugha za asili za makabila mbalimbali nchini kwa lengo la kuziendeleza.
Idara ya Maendeleo ya Sanaa
Idara ya Maendeleo ya Sanaa imeundwa baada ya muundo mpya wa Wizara. Kabla ya hapo Idara ilikuwa ni sehemu ndani ya Idara ya Maendeleo ya Utamaduni. Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 idara ilitekeleza majukumu yake ikiwa pamoja na Idara ya Maendeleo ya Utamaduni.
Idara ya Sanaa ndiyo yenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya Sekta ya Sanaa nchini. Sanaa hizo ni pamoja na filamu, muziki, michezo ya kuigiza, ngoma, dansi, sarakasi na kazi za mikono kama vile uchoraji, uchongaji, uhunzi, usukaji, ufumaji, ushonaji na ususi.
Idara ya Sanaa inajukumu la kusimamia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) na Bodi ya Filamu Tanzania.
Idara ya Maendeleo ya Sanaa imegawanyika katika kuu sehemu mbili;-
2. Sehemu ya haki na Maendeleo ya wasanii (Sehemu hizi zitaongozwa na Wakurugenzi wasaidizi wawili 2)
MAJUKUMU YA IDARA YA MAENDELEO YA SANAA
Majukumu ya Idara ya Maendeleo ya Sanaa ni haya yafuatayo;-
I.Kusimamia na kuratibu uandaaji wa Sera ya Maendeleo ya Sanaa.
II.Kuandaana kutoa miongozo ya kusimamia utekelezaji wa shughuli za Sanaa na Ubunifu.
III.Kuendeleza, kufuatilia, kutathmini na kurekebisha utekelezaji waSheria na Miongozo ya Sera ya Sanaa,
- MAJUKUMU YA SEHEMU YA URATIBU WA TASNIA YA SANAA
Majukumu ya Sehemu ya Uratibu wa Tasnia ya Sanaa ni:-
i.Kuendeleza, Kuratibu na kutekeleza mbinu za kiutendaji za shughuli za sanaa .
ii.Kuendeleza, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera ya kitaifa ya sanaa, sheria na miongozo katika muziki, sanaa za maonesho na ubunifu kwa ujumla.
iii.Kudhibiti na kusisitiza matumizi ya maadili ya kitaifa katika shughuli za muziki, sanaa za maonesho na ubunifu kwa jumla .
iv.Kuratibu na kuendeleza mifumo ya kutambua na kutoa tuzo kwa wasanii na taasisi bora katika kutekeleza shughuli za maendeleo ya sanaa.
v.Kuratibu na kusimamia taasisi za sanaa za Tanzania, wanamuziki, sanaa za maonyesho, na wataalamu wa sanaa wanaofanya vizuri katika Tasnia.
vi.Kufuatilia na kutathmini majukumu nakazi ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuba), bodi ya Ukaguzi wa filamu na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
vii.Kuratibu na kusimamia nakutoa miongozo yautekelezaji wa Sera ya Taifa ya filamu. MAJUKUMU YA SEHEMU YA HAKI NA MAENDELEO YA WASANII.
Majukumu ya Sehemu ya haki na Maendeleo ya Wasanii ni:-
i.Kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa Programu mbalimbali za wasanii.
ii.Kuratibu na kusimamia mikataba ya wasanii na kazi zao
iii.Kuratibu na kutoa ujuzi wa ujasiriamali na kitaaluma.
iv.Kuratibu, kubuni na kutekeleza miradi ili kukuza wasanii na kazi zao.
v.Kuratibu makundi ya sanaa, vyama na mashirikisho.
vi.Kuratibu, kusimamia, kudhibiti na kutoa miongozo ya ulinzi wa kazi za wasanii ikiwa ni pamoja na haki miliki.
vii. Kuratibu na kufuatilia haki za wasanii kwa kushirikiana na taasisi inayohusikana hakimiliki na hakishiriki.
Idara ya Maendeleo ya Michezo
To provide expertIDARA YA MAENDELEO YA MICHEZO
1.Utangulizi
Sekta ya Michezo hapa nchini imekuwa ikisimamiwa na Sera ya Maendelo ya Michezo yam waka 1995. Malengo ya Sera hiyo ni pamoja na kuhamasisha Umma wa Watanzania kushiriki katika Michezo na mazoezi ya viungo; kuwezesha upatikanajio wa Viwanja na zana bora na za kutosha kwa ajili ya kuimarisha Maendeleo ya Michezo nchini, kuandaa na kutayarisha wataalamu wa kutosha katika fani na taaluma mbali mbali za Michezo ya Kimataifa. Malengo mengine ni kuimarisha ushirikiano wa Kimataifa katika utoaji wa Elimu kwa Michezo na kuimarisha utafiti katika Michezo ya jadi kwa lengo la kuiendeleza. Idara ya Maendeleo ya Michezo ndipyo chombo cha juu cha Wizara ambacho kinasimamia utekelezaji wa Sera hiyo hapa nchini Tanzania.
2.Majukumu ya Idara ya Maendeleo ya Michezo.
Katika kuhakisha Tanzania inanufaika na Sekta ya Michezo, Serikali ilitunga Sera ya Maendeleo ya Michezo yam waka 1995 ambayo ilibainisha malengo mbali mbali ya kutekelezwa kupitia mgawanyo wa majukumu yaliyobainishwa na Sera hiyo kama ifuatavyo:
(i)Uhamasishaji kwa Umma wa Tanzania kushiriki katika Michezo na mazoezi ya viungo vya mwili
(ii)Upatikanaji wa viwanja vya kutosha kwa ajili ya kuimarisha maendeleo ya Michezo
(iii)Upatikanaji wa zana bora za Michezo ili kuimarisha Michezo
(iv)Uuandaaji na utayarishaji kwa Wataalamu wa kutosha katika fani na taaluma mbali mbali za Michezo
(v)Kuhakikisha Timu na wachezaji wanafanya vizuri katika Michezo na Mashindano ya Kimataifa
(vi)Utafiti katika Michezo ya Jadi kwa lengo la kuifufua na kuindeleza.
(vii)Ushirikiano na Mataifa mengine katika utoaji wa Elimu kwa Michezo na Michezo
(viii)Mgawanyo wa Majukumu katika utekelezaji wa Sera
3.Muundo wa Idara ya Maendeleo ya Michezo
Idara ya Maendeleo ya Michezo imegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni sehemu ya maendeleo ya Michezo na sehemu inayoshughulikis maendeleo ya miundo mbinu ya Michezo. Kwa mujibu wa Muundo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Micheo. Idara ya Maendeleo ya Michezo ina Taasisi mbili ambazo zinafanya kazi na Idara. Taasisi hizo ni; chuo cha Maendeleo ya Michezo Mlya na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
i.Baraza la Michezo la taifa ni Taasisi iliyoundwa kwa ksheria ya Bunge ya Na.12 ya mwaka 1967. Kwa mujibu wa sheria hiyo Baraza lina majukumu yafuatayo
ii.Kuvisaidia na kuviendeleza vyama vya Michezo kwa kuandaa mafunzo kwa viongozi wa vyama na vilabu vya Michezo
iii. Kutoa ushauri kwa vyama vya Michezo juu ya ujenzi wa viwanja vya Michezo
iv.Kutafuta vifaa vya Michezo na kuvisambaza kwa wanaohitaji
v.Kuandaa utaratibu wa kujenga uhusianio wa kimichezo kati ya Vyama vya Michezo na Wachezaji wenyewe
vi.Kuchambua na kuthibitisha ratiba za masshindano ya Michezo zinazoandaliwa na vyama vya Michezo
vii.Kuandaa Tamasha la Michezo kitaifa kwa kushirikiana na vyama vya Michezo
viii.Kuishauri Wizara juu ya uhusiano wa kimichezo na Mataifa mengine
ix.Kuandaa na kutekelez mbinu mbali mbali za kusisimua mwamko wa Michezo kwa ujumla, kama vile kutenegeza na kutoa medali za Michezo, kutoa misaada au nafasi za mafunzo ya Michezo (Scholarship), kuendesha zahanati za Michezo
x.Kuhakikisha kuwa fedha za vyama vya Michezo zinakaguliwa na matumizi mabaya ya fedha yanaondolewa katika vyama hivyo.ise and services in policy formulation, implementation, monitoring and evaluation
Administration and Human Resource Management Division
Objectives
To provide expertise and services on human resources management and administrative matters to the Ministry.
Functions
To provide strategic inputs to management on Administration and Human resources Management issues
To provide link between the Ministry and the President’s Office Public Service Management on operationalization of the Public Service Management and Employment Policy of 1998 and Public Service Act No. 8 of 2002
The Division is led by the Director and comprise two Sections as follows;
Administration Section
Human Resources Management Section
Idara ya Sera na Mipango
1. UTANGULIZI
Idara ya Sera na Mipango inatekeleza majukumu yake kupitia Sehemu ya Sera, Sehemu ya Mipango na Bajeti na Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathimini.
2. MAJUKUMU YA IDARA YA SERA NA MIPANGO
Kazi kuu ya Idara hii ni kuratibu shughuli zote zinazotekelezwa na Wizara. Aidha, Idara hii hutoa utaalamu na huduma kwa masuala ya utungaji, utekelezaji, kufuatilia na kutathmini Sera za Wizara. Vilevile, Idara hii ni kiunganishi kati ya Idara na Vitengo vyote Wizarani. Majukumu mengine ni pamoja na:
i Kuratibu utungaji wa Sera za Wizara, kufuatilia utekelezaji wake na kufanya tathimini;
ii Kuchambua nyaraka mbalimbali kutoka Asasi nyingine na kushauri juu ya nyaraka hizo;
iii) Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mipango na Bajeti ya Wizara;
iv) Kufanya Ufuatiliaji na Tathimini ya Mipango na Bajeti na kuandaa taarifa ya utekelezaji;
v Kufanya utafiti, tathimini ya mipango ya Wizara na kutoa uamuzi wa mwelekeo wa mbele wa Wizara;
vi Kumotisha na kuwezesha utoaji wa huduma kwa Wizara kwa kutumia sekta binafsi;
vii) Kuratibu maandalizi ya michango ya Hotuba za Bajeti na Taarifa za Uchumi za mwaka za Wizara;
viii) Kujenga uwezo wa Mpango Mkakati, Bajeti, Ufuatiliaji na Tathimini katika Wizara; na
ix Kuhakikisha kuwa Mipango na Bajeti za Wizara inajumuishwa katika Mipango na Bajeti za Serikali
3. UONGOZI NA UTAWALA
Idara ya Sera na Mipango inaongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango na kusaidiwa na Wakurugenzi Wasaidizi kwa kila sehemu.
Procurement and Supply
Kuwezesha shughuli za Ununuzi na Ugavi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo ili kukidhi mahitaji na huduma stahiki ndani ya Wizara.