Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika ("CAF"), kwa kushauriana na Mataifa matatu yatakayoandaa Michuano ya CAF ya Mataifa ya Afrika mwaka huu Kenya, Tanzania na Uganda (CHAN) 2024 wametangaza viwanja vitakavyoandaa Mechi ya Ufunguzi, Nafasi ya Tatu na Nne na Mechi ya Fainali ya Mashindano hayo. Michuano ya CAF ya Mataifa ya Afrika Kenya, Tanzania na Uganda (CHAN) 2024 itafanyika kati ya 02 - 30 Agosti, 2025, kuashiria kurejea katika ardhi ya Afrika Mashariki kufuatia michuiano ya 2016 nchini Rwanda. Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi ya michuano ya CAF ya Mataifa ya Afrika Kenya, Tanzania na Uganda (CHAN) 2024 tarehe 02 Agosti 2025.