Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Majukumu ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
- Kuratibu mikutano ya Wizara na vyombo vya habari juu utoaji wa taarifa kwa umma kuhusu masuala yote ya kihabari ya Wizara;
- Kuratibu masuala yote ya Mawasiliano ndani ya Wizara;
- Kuandaa vipindi katika vyombo vya habari, kusambaza taarifa na machapisho mbalimbali yanayoelimisha Umma kuhusu Sera, Sheria, programu, maonyesho, na maboresho mbalimbali yanayofanyika na kutekelezwa na Wizara;
- Kuandaa na kutekeleza Mkakati wa Mawasiliano wa Wizara;
- Kuratibu na kuandaa habari na uzalishaji wa makala zinazohusu Wizara na kuzisambaza kwenye vyombo vya habari yakiwemo magazeti, majarida, radio, Televisheni na mitandao ya kijamii;
- Kuhuisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za Idara za kisekta kwenye tovuti ya Wizara;
- Kuwasiliana na wananchi pamoja na vyombo vya habari pamoja na kushughulikia hoja mbalimbali za wadau zinazoihusu Wizara kwenye Magazeti na Mitandao ya kijamii;
- Kushiriki katika maandalizi ya nyaraka mbalimbali za kihabari za sekta za wizara kwa ajili ya warsha na mikutano;
- Kuratibu na kuandaa Makala (print and electronic) na majarida ya Wizara; na
- Kuhifadhi taarifambalimbali za Wizara.