Majukumu ya Wizara
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ina Majukumu yafuatayo:
- Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sera za Sekta ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo.
- Kuendeleza, kuwezesha na kuratibu masuala ya kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara.
- Kusimamia na kuratibu Maendeleo ya Sekta ya Habari nchini.
- Kusimamia na kuratibu Maendeleo ya Utamaduni nchini.
- Kusimamia na kuratibu Maendeleo ya Sanaa nchini.
- Kusimamia na kuratibu Maendeleo ya Michezo nchi.
- Kusimamia utendaji wa Taasisi, Mashirika ya Umma, Wakala, Miradi na programu zilizo chini ya Wizara.