Maendeleo ya Utamaduni
Idara ya Maendeleo ya Utamaduni inatekeleza Sera za Utamaduni ya mwaka 1997 pamoja na Malengo yake.
Malengo:
- Kushirikisha shughuli za Utamaduni wa Taifa kuanzia Shule za Awali, Sekondari na Elimu ya Juu na kuhakikisha kwamba mafunzo ya Utamaduni yanaingizwa katika Mitaala na muhtasari na kufundishwa shuleni na vyuoni.
- Kuhimiza na kukuza utaifa kwa vijana wetu na wananchi kwa ujumla.
- Kuhimiza Utu katika Maendeleo ya Taifa.
- Kuimarisha Uchangiaji wa gharama, Ukuzaji, Utunzaji na Uimarishaji wa Taasisi za Utamaduni kwa watumiaji wa huduma hizo.
- Kuelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Utamaduni na jinsi sanaa inavyoweza kutumika katika kupambana na UKIMWI.
Majukumu:
- Kutunga na kusimamia, kutathmini na kupitia utekelezaji wa sera za maendeleo ya utamaduni sheria,kanuni na miongozo mbali mbali.
- Kusimamia na kuratibu utendaji kazi wa taasisi za kiutamaduni zilizo chini ya wizara.
- Kuanzisha na kuibua programu za ushirikiano na ubadilishanaji wa maarifa,uzoefu na ujuzi wa kiutaduni baina ya Tanzania na Mtaifa mengine.
- Kutoa tuzo kwa kazi za utamaduni kupitia matukio ya kiutamaduni.
- Kutoa miongozo mbalimbali kuhusiana na misingi ya maadili ya Taifa.
- Kukuza,kuwezesha na kuratibu ujenzi wa uwezo wa rasilimali watu ya kiutamaduni kwa kushirikiana na waajiri wa karibu.
- Kuanzisha mbinu za kuendeleza, kutangaza masuala ya mila, desturi na lugha;
- Kutoa ushauri juu ya masuala yanayohusiana na maadili katika kuandaa sinema, filamu/uigizaji, maonesho na utoaji wa leseni katika maeneo hayo.
- Kuratibu na kushiriki matukio, semina, warsha, makongamano na mafunzo mbalimbali yanayohusu utamaduni na lugha.
- Kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa watendaji wa kazi za utamaduni.
Idara ya Maendeleo ya Utamaduni ina sehemu kuu mbili:
- Sehemu ya urithi wa utamaduni na maadili ya Taifa.
- Sehemu ya Lugha.