Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Kuundwa kwa Wizara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alianzisha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Tangazo la Serikali Na.782 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali la tarehe 22 Novemba, 2021 kama ilivyofanyiwa marekebisho kwa Notisi ya Serikali ya tarehe 17 Januari, 2025. Katika kutekeleza majukumu yake kikamilifu, Wizara kimuundo imegawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo ni:

  1. Usimamizi na utekelezaji wa masuala ya kisekta
  2. Uendeshaji, uratibu na usimamizi

USIMAMIZI NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA KISEKTA

Eneo hili linatekelezwa na Idara ya Habari, Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Idara ya Maendeleo ya Sanaa na Idara ya Maendeleo ya Michezo kwa ushirikiano na Taasisi zilizopo chini ya Idara hizo.

UENDESHAJI URATIBU NA USIMAMIZI

  • Eneo hili linatekelezwa na Idara ya Sera na Mipango, Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Kitengo cha Fedha na Uhasibu, Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Kitengo cha Huduma za Sheria, Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini pamoja na Kitengo cha Tathmina na Ufuatiliaji.
  • Kuendeleza utambulisho wa Taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa Habari, Kukuza Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Maendeleo ya Jamii na Uchumi.