Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Kitengo cha TEHAMA

Majukumu ya Kitengo cha TEHAMA .

Kitengo hiki kinatekeleza majukumu muhimu yanayolenga kuhakikisha matumizi bora ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ndani ya Wizara, kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa Serikali. Majukumu ya kitengo hiki ni pamoja na:

  1. Kutekeleza Sera ya TEHAMA na Serikali Mtandao:
    Kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wa sera, miongozo na viwango vya TEHAMA vinavyotolewa na Serikali, ili kuwezesha utoaji wa huduma kwa njia ya kielektroniki.
     
  2. Kutengeneza na Kuratibu Mifumo ya TEHAMA Wizarani:
    Kubuni, kutengeneza na kusimamia mifumo ya kompyuta inayotumiwa na wizara ili kurahisisha shughuli za kila siku za kiutendaji.
     
  3. Kuhakikisha Kompyuta na Programu Zinafanya Kazi Vizuri:
    Kusimamia ufungaji na uendeshaji wa vifaa vya TEHAMA, ikiwa ni pamoja na matengenezo ya kompyuta, programu na mitandao ya ndani ya Wizara.
     
  4. Kuandaa Mahitaji kwa Ajili ya Ununuzi wa Vifaa vya TEHAMA:
    Kubaini mahitaji ya vifaa na huduma za TEHAMA, na kuandaa nyaraka za manunuzi kwa mujibu wa taratibu za Serikali.
     
  5. Kusimamia Mifumo ya Serikali Wizarani:
    Kusimamia Mifumo yote Serikali inayotumiwa na Watumishi wa Wizara na kuhakikisha inafanya kazi kwa ufanisi na usalama.
     
  6. Kufanya Tafiti na Kushauri Katika Matumizi ya TEHAMA:
    Kufanya tafiti kuhusu teknolojia mpya na kutoa ushauri juu ya matumizi bora ya TEHAMA ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa haraka na kwa viwango vya juu.