Kitengo cha Huduma za Sheria
Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:-
Kutoa huduma za kisheria na usaidizi wa kisheria kwa Idara na Vitengo vya Wizara, Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kutafsiri sheria, masharti ya Mikataba, Mikataba ya kimataifa, Mikataba ya ubinafsishaji, Mikataba ya manunuzi, Dhamana, Barua za ahadi, Hati za Makubaliano ya Ushirikiano, Mikataba ya ushauri na aina nyingine za Mikataba na Hati nyingine za kisheria.
- Kutoa utaalamu wa kisheria katika kuandaa Sheria ikiwemo kutunga Sheria za Bunge na Kanuni na kuziwasilisha katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuuu wa Serikali.
- Kusimamia majadiliano ya Mikataba katika maendeleo ya sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo
- Kutoa msaada na huduma za kisheria kwa Wizara na Taasisi zake
- Kushiriki katika majadiliano mbalimbali na mikutano inayohitaji utaalamu wa kisheria katika sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.
- Kutafsiri Sheria za sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo
- Kuwasiliana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu mashauri ya kesi za madai na madai mengine yanayoihusu Wizara na;
- Kutoa utaalamu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu mapitio ya Hati / nyaraka za kisheria kama Hati idhini, Notisi, Vyeti, Mikataba na Hati za Uhamisho.