News

Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) watembelea na kufanya ukaguzi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 5, 2024.
Viongozi hao wapo nchini kwa takriban siku mbili kuanzia Oktoba 5 kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa viwanja mbalimbali vitakavyotumika kwenye mashindano ya CHAN 2025.
Aidha, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gerson Msigwa aliwakaribisha viongozi hao huku akiwahidi ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini.
Maofisa hao wa CAF, wameriidhishwa na hatua iliyofikiwa ya Maandalizi na kupongeza juhudi za Serikali pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa utayari wao katika mashindano hayo, ambapo Tanzania, Kenya na Uganda ndio wenyeji.