News
Press Release
News

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameiagiza Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kujiandaa vyema kwa ajili ya mashindano ya Samia Taifa Cup ambayo yatafanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Mhe. Ndumbaro ametoa maagizo hayo Septemba 21, 2023 Zanzibar wakati akikabidhivifaa vya michezo kwa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya maandalizi yamashindano hayo ambayo yatahusisha michezo mbalimbali.
"Mwaka huu mashindano yatajumuisha pia Zanzibar na kutakua na Mashindano ya Muziki wa Kizazi Kipya. Lengo la mashindano haya ni kuendelea kuenzi Muungano wetu nakuhakikisha jamii inajishughulisha na michezo, Sanaana Utamaduni kwakua ni Sekta ambazo zinaibua vipaji na kutoa fursa ya ajira" amesema Mhe. Ndumbaro.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita amesemavifaa hivyo vitagawiwa katika mikoa yote ya Zanzibar na mashindano yataanzia katika ngazi ya Shehia mpaka Mkoa ili kupata wawakilishi wazuri Kitaifa.
Miongoni mwa vifaa alivyokabidhi Mhe. Ndumbaro ni pamoja na mipira yamichezo ya mpira wa Miguu, Kikapu na Wavu ambayo kila mchezo mipira 18 huku akiwakaribisha wadau kuiunga mkono jambo hilo katika michezo mingine.