News

Posted On:: Sep, 22 2023
News Images

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Septemba 20, 2023 Jijini Dar es Salaam amekutana na viongozi wa timu ya Simba ambapo wamejadili masuala mbalimbali yakiwemo maendeleo ya michezo nchini.

Kikao hicho pia kimejadili maandalizi ya michuano ya Africa Football League ambayo timu ya Simba inashiriki ikiwa miongoni mwa timu nane bora Afrika.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Ally Mayayi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha, Katibu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini Bw. Wilfred Kidau, Mtendaji Mkuu wa Timu ya Simba Bw. Iman Kajula pamoja na viongozi wengine