News

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Akson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Usiku wa Taarabu Julai 03, 2022 utakaofanyika katika Fukwe za Coco (CoCo Beach) Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 29, 2022, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amesema usiku utahusishamuziki wa taarabu asilia na taarabu ya kisasa kutoka ndani na nje ya nchi
“usiku huu utapambwa na mbalimbali akiwemo Mzee Yusuph, Hadija Kopa, Patricia Hillary, Isha Mashauzi, Sabaha Mchacho, Abdul Misambano na wengine wengi" alisema Mhe. Makalla.
Ameongeza kuwa, vikundi mbalimbali ikiwemo First Class , Wana Nakshi Nakshi, Rahat Zaman, Nadi Ikhwan Safaa, Chama Cha Wasanii wa Muziki Zanzibar pamoja na Vikundi vya taarabukutoka nchiniBurundi, Kenya, na. Visiwa vya Comoro vitashiriki
Usiku huo wa taarabu ni muendelezo wa Tamasha la Utamaduni la Kwanza Kitaifa ambalo litafanyika katika Uwanja wa Uhuru Julai 01 hadi 03, 2022 ikiwa ni kuelekea kilelele cha maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani Julai 07, 2022.