News
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa matamasha mbalimbali ya sanaa nchini yanapaswa kuwa mengi sababu yanafanya Watanzania kuwa na furaha wakati wakitafuta hela kuijenga nchi.
Mhe. Mwinjuma amesema hayo kwenye utambulisho wa album ya Wasanii wa hiphop Tanzania Farid Kubanda (Fid Q) na Isack Maputo (Lord Eyes) iitwayo NENO iliyofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha Utamaduni cha Urusi jijini Dar es salaam Novemba 2, 2024.
Akiwasilisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Mwinjuma amesema "Rais Samia anafurahia kuona Watanzania wanafurahi kupitia Sanaa ya nchi yao na sisi kama Wizara tutahakikisha hivi vitu havikwami sehemu yoyote na vitaungwa mkono kwa asilimia mia"
Fid Q na Lord Eyes wameonjesha vionjo vya nyimbo saba kati ya kumi na tano zilizopo kwenye album yao iitwayo NENO. Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mabalozi mbalimbali, Wasanii, Waandishi wa habari, pamoja na Wadau wa Sanaa.