News

Posted On:: Sep, 26 2024
News Images

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema kuwa, Mkakati wa Taifa wa miaka kumi wa Kubidhaisha lugha ya Kiswahili wa mwaka 2022 hadi 2032 unatarajia kufunguliwa kwa vituo takriban mia moja nje ya nchi.

Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo Septemba 25, 2024 wakati akifunga mafunzo ya Waandishi waendesha Ofisi Mkoani Morogoro yaliondaliwa na Baraza la Kiswahili Tanzania ambapo aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Methusela Ntonda

"Mkakati huo una lengo la kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa bidhaa kwa kutoa fursa za kujikwamua kiuchumi kwa rasilimaliwatu wanaojihusisha na lugha hii pamoja na watoa huduma za Kiswahili" amesema Mhe. Mwinjuma.

Miongoni mwa mambo yanayolengwa katika mkakati huo ni kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Hivyo, kwa kutambua umuhimu wa waandishi waendesha ofisi na kwa kuzingatia maelekezo ya Waziri Mkuu, wamewapa kipaumbele kwa kuanza kutoa mafunzo hayo na ameahidi kuwa mafunzo yatakuwa endelevu kwa kutolewa kila mwaka mara moja.

Lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha nyaraka za serikali na mawasiliano kati ya ofisi moja na nyingine yanazingaz¡tia matumuzi mazuri ya lugha na hivyo kufanya Tanzania idhihirishe kwa vitendo kuwa ni kinara wa Kiswahili.