News
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwijuma amezindua Mashindano ya Mathayo CUP katika Jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimanjaro lililoandaliwa na Mbunge wa Same Magharibi, Mhe. Mathayo David.
Akizindua mashindano hayo Novemba 26, 2023 Mhe. Mwinjuma amempongeza Mbunge huyo, kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yanatoa fursa kwa vijana kuonesha vipaji na kuongeza uchumi kufuatia zawadi watakazopata katika mashindano hayo.
Katika kuhamasisha wananchi kushiriki michezo hiyo, Mhe. Mwinjuma alitumia usafiri wa Helkopter katika kufikia Tarafa zote tatu kwa haraka iliyotolewa na mdhamini wa mashindano hayo Mhe. Mathayo
Kwa upande wake Mbunge Mhe. Mathayo amesema mashindano hayo yameanza kwenye tarafa ambapo
mshindi wa kwanza atazawadiwa Shilingi Milioni mbili, wa pili milioni 1.2, na mshindi wa tatu milioni 1.
Amesema kwa upande wa Jimbo mshindi wa jumla atapata Milioni 5, pamoja na Kombe, mshindi wa pili milioni 4 na mshindi wa tatu milioni 3.