News

Posted On:: May, 17 2024
News Images

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ameshuhudia mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya Kamati ya Utendaji ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) dhidi ya Wajumbe wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) iliyofanyika leo Mei 16, 2024 Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ambao ni sehemu ya muhula wa 79 wa mkutano mkuu wa baraza hilo umefanyika kwa lengo la kuitumia michezo kuimarisha utimamu wa mwili na kueneza amani Duniani.