News

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Anatarajiwa kuwa mgeni wa Rasmi katika Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili ambalo litafanyika Jijini Havana Nchini Kuba kuanzia Novemba 7 hadi 10, 2024.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro katika mkutano wake na waandishi wa habari Oktoba 30, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Ndumbaro amesema kuwa Lugha ya Kiswahili imefanikiwa kutambuliwa na UNESCO kama Lugha ya 7 ya kimataifa, ikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 500 duniani, hivyo ni wakati wa kukipeleka katika mataifa mbalimbali hapa Duniani kwa ajili ya kukibidhahisha.
Aidha, Dkt Ndumbaro amesema uamuzi wa kufanyia Kongamano hilo Nchini Kuba ni kwa sababu nchi hiyo ni miongoni mwa Jamii zinazozungumza kispaniola ambapo sasa Lugha ya kiswahili itabidhahishwa kwenda hadhira ya Kispaniola pia itaendelea kwenda mataifa mengine na Lugha nyingine.
Katika kongamano hilo ambalo litatanguliwa na Ufunguzi rasmi kutoka Mhe. Rais Dkt Samia na mwenyeji wake Rais wa Kuba Mhe. Miguel Diaz - Canel pia kutakuwa na Semina mbalimbali, pamoja na Uzinduzi wa Kamusi ya Kiswahili kwenda katika Lugha ya Kispaniola ambayo imeandaliwa na chuo kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM)
Katika hatua nyingine, Kongamano Hilo linatarajiwa kuwa na washiriki 600 kutoka Nchi mbalimbali Duniani, Taasisi Binafsi,wadau kutoka vyuo vikuu na vyama vya kiswahili ambao hawa watajigharamia wenyewe kwa kila kitu huku vikundi mbalimbali vya burudani vikitarajia Kupamba Kongamano hilo.