News

Posted On:: Feb, 26 2024
News Images

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali ina mpango wa kufufua vituo vya michezo vilivyofungwa ili kuendeleza shughuli za michezo sambamba na kukuza na kuibua vipaji

Mhe. Ndumbaro amesema hayo Februari 23, 2024 alipokutana na viongozi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kujadiliana juu maendeleo ya sekta ya michezo katika mkoa huo na kutembelea nyumba ya Wizara aliyokua akiishi mkuu wa kituo hicho cha Michezo kabla ya kufungwa mwaka 2016.

Mpango huo unakuja kuelekea uenyeji wa Tanzania, Kenya na Uganda katika Fainali za mataifa ya Afrika AFCON 2027 ambapo vituo hivyo vitatumika kama sehemu za kuibua vipaji kwa vijana.

Aidha Mhe. Ndumbaro amesema serikali itafungua vituo vingine vya Michezo katika maeneo mbalimbali ili kuongeza wigo wa kuibua vipaji