News

Posted On:: Dec, 05 2024
News Images

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Urusi zimepanga kuandaa filamu maalumu ya kuonesha mchango uliotolewa na nchi hizo katika uhuru wa nchi mbalimbali za Afrika.

Hayo yamejiri kufuatia ziara ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro nchini Urusi, ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Utamaduni wa nchi hiyo Mhe. Olga Lyubimova hivi karibuni jijini Moscow.

Viongozi hao wamesema, kupitia filamu itakayoandaliwa na wasanii wa pande zote mbili itasaidia kuonesha kizazi kipya ni kwa jinsi gani mataifa hayo yalitoa mchango wao kwa ukombozi wa nchi za Afrika.

Wamekubaliana pia, kuanzisha ushirikiano katika matukio mbalimbali ya utamaduni ya pande zote mbili ikiwemo kubadilisha utaalamu katika matukio hayo ikiwemo tamasha la kitaifa la utamaduni linalofanyika nchini kila mwaka.