News

Posted On:: Aug, 15 2024
News Images

Tanzania na Uswisi zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika kukuza na kuendeleza sekta za utamaduni, sanaa na michezo.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa kikao kati ya Waziri wa Uatamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mhe.Didier Chasot, kilichofanyika ofisi za wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.

Waziri Dkt. Ndumbaro amemshukuru Balozi Didier kwa mchango mkubwa wa Serikali ya Uswizi katika kusaidia ukuaji wa Sekta ya Utamaduni hapa nchini kupitia programu mbalimbali za ushirikiano.

"Tanzania na Uswisi zimekuwa na uhusiano wa kipekee kwa muda mrefu hususani kwenye sekta ya utamaduni ulionufaisha wadau wa sekta hiyo, hivyo Tanzania inajivunia na itaendeleza uhusiano huo" alifafanua Waziri Dkt. Ndumbaro.

Kwa upande wake Balozi Didier amemshukuru Waziri Dkt. Ndumbaro kwa ushirikiano aliompatia katika kipindi chake hapa nchini na kwamba Serikali ya Uswisi kupitia ubalozi wake hapa nchini itaendelea kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa inasaidia kukumilisha mpango wa uhuhushaji wa Sera ya Utamaduni.

Balozi Didier Chasot yupo katika ziara ya kuaga viongozi wa serikali mara baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka minne nchini Tanzania.