News

Posted On:: Sep, 17 2023
News Images

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amefanya ziara Uwanja wa Benjamin Mkapa hivi Septemba 17, 2023 jijini Dar es salaam kujionea ukarabati wa uwanja huo ambao utatumika kwenye ufunguzi wa michuano ya African Football League Oktoba 20, 2023.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ukarabati wa Uwanja huo Bw. Abel Shirima ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema taa za uwanja huo zote zimetolewa na hatua inayofuata ni kutandaza nyaya za umeme ili kufunga taa mpya za uwanja huo.

Ziara ya Katibu Mkuu huyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro aliyotoa hivi karibuni kutaka ukarabati wa uwanja huo ukamilike ifikapo Oktoba 15, 2023.