News

Posted On:: May, 20 2024
News Images

Timu ya Netiboli ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoshana nguvu na timu ya Muungano ya Jijini Dodoma kwa kupata sare ya goli 19 katika mchezo uliochezwa Mei 18, 2024 uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.

Katika mchezo huo uliokua na ushindani mkubwa huku ukishuhudiwa na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Savera Salvatory, Timu ya Utamaduni imeonesha uwezo mkubwa katika eneo la kati dhidi ya wapinzani wao.

Mchezo huo umetanguliwa na mazoezi ya viungo na mbio fupi, ikiwa ni muendelezo wa watumishi wa wizara hiyo kufanya mazoezi kila jumamosi kuunga mkono maelekezo ya viongozi wakuu wa nchi.