News

Posted On:: Nov, 30 2023
News Images

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Baraza la Uhusiano wa Utamaduni la India (ICCR) Dkt. Vinaya Sahasrabuddhe aliyeambatana na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Srinkanta Pradhan kuhusu utekekezaji wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini India hivi karibuni.

Kikao hichokimefanyika Novemba29, 2023 jijini Dar es salaam ambapokimejikita katika kuchambua na kujadili jinsi ya kutekeleza kwa vitendo makubaliano yaliyotiwa saini kati ya Tanzania na India kuhusu Mpango wa Ushirikiano wa Masuala ya Utamaduni uliosainiwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Oktoba 9, 2023 nchini India.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.Bw. Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Idara Maendeleo ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dkt. Kiagho Kilonzo na viongozi wengine wa wizara.