News

Posted On:: Dec, 05 2022
News Images

Wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva na Singeli usiku wa tarehe 4 Desemba, 2022 wamenogesha hafla ya utoaji tuzo za UNI AWARDS, hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam na kuwakosha mamia ya wanafunzi waliohudhuria kutoka vyuo mbalimbali nchini.

Wasanii hao maarufuni Maarifa, Dulla Makabila na Dogo Janja.

Mgeni rasmi alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Dkt. Kedmon Mapana ambaye alimuwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa.