News

Posted On:: May, 17 2024
News Images

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ametoa rai kwa watanzania waishio nje ya nchi kutangaza Utamaduni wa Tanzania ikiwemo lugha ya Kiswahili.

Mhe. Ndumbaro ametoa rai hiyo Mei 16, 2024 katika Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Tanzania kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China linaloendelea Beijing China.

Ametumia nafasi hiyo kueleza Utamaduni wa ushabiki wa jadi uliopo baina ya timu mbili Kongwe nchini za Simba na Yanga ambazo zinafuatiliwa na washabiki wengi Afrika Mashariki.

Siku hiyo ya Utamaduni imehudhuriwa pia na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki, Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas na Viongozi na maafisa wengine wa Serikali, imepambwa na maonesho mbalimbali ya Utamaduni wa Tanzania pamoja na burudani kutoka kwa wasanii.