Habari
KAMATI YA BUNGE YAPOKEA NA KUJADILI MAJUKUMU YA WIZARA YA HABARI
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepokea na kujadili taarifa kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Taasisi zake.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Husna Sekiboko imepokea taarifa hiyo, leo Januari 20, 2026 Bungeni jijini Dodoma ambayo imewasilishwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Hamis Mwinjuma.
Mhe. Mwinjuma ameeleza majukumu ya kisera na kiutendaji yanayotekelezwa wizarani hapo pamoja na miradi ya maendeleo.
