Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

CAF CHAN 2024: Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mechi ya Ufunguzi


Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika ("CAF"), kwa kushauriana na Mataifa matatu yatakayoandaa Michuano ya CAF ya Mataifa ya Afrika mwaka huu Kenya, Tanzania na Uganda (CHAN) 2024 wametangaza viwanja vitakavyoandaa Mechi ya Ufunguzi, Nafasi ya Tatu na Nne na Mechi ya Fainali ya Mashindano hayo.

Michuano ya CAF ya Mataifa ya Afrika Kenya, Tanzania na Uganda (CHAN) 2024  itafanyika kati ya 02 - 30 Agosti, 2025, kuashiria kurejea katika ardhi ya Afrika Mashariki kufuatia michuiano ya 2016 nchini Rwanda.

Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi ya michuano ya CAF ya Mataifa ya Afrika Kenya, Tanzania na Uganda (CHAN) 2024 tarehe 02 Agosti 2025.

Uwanja wa Mandela mjini Kampala, Uganda umeteuliwa kuandaa mechi ya tatu na ya nne ya michuano hiyo.

Uwanja wa Kasarani wa Kenya jijini Nairobi utaandaa mechi ya Fainali ya Mashindano hayo tarehe 30 Agosti 2025. 

Mataifa mwenyeji:

  • Mechi ya Ufunguzi  itaandaliwa Dar es Salaam, Tanzania Siku ya Jumamosi, 02 Agosti.
  • Mechi ya Fainali itafanyika Nairobi, Kenya  Jumamosi, 30 Agosti.
  • Mechi ya Nafasi ya Tatu itaonyeshwa Kampala, Uganda.

Zaidi ya hayo, Zanzibar imeteuliwa kuwa mojawapo ya Maeneo ya Waandaji - uamuzi ambao unasisitiza dhamira ya CAF ya kupanua ufikiaji na ujumuishaji wa soka la Afrika. Uwanja wa Amaan Zanzibar hivi karibuni ulifanikiwa kuandaa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF 2024/25 iliyofana ya mwezi Mei mwaka huu 2025.

Miji Wenyeji wa Hatua za Makundi za Mashindano hayo ni kama ifuatavyo:

  • Kundi A | Nairobi, Kenya: Kenya, Morocco, Angola, DR Congo, Zambia
  • Kundi B | Dar es Salaam, Tanzania: Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, Jamhuri ya Afrika ya Kati
  • Kundi C | Kampala, Uganda: Uganda, Niger, Guinea, Afrika Kusini, Algeria
  • Kundi D | Zanzibar: Senegal, *Congo, Sudan, Nigeria

*Kufuatia uamuzi wa Bodi ya Rufaa ya CAF, nafasi ya Equatorial Guinea ilichukuliwa na Congo.

Kwa maelezo zaidi kuhusu michuano ya CHAN ya Mataifa ya Afrika, tafadhali tembelea https://www.cafonline.com/caf-african-nations-championship/