Habari
SINGELI MBIONI KUTAMBULIKA KAMA URITHI WA TAIFA UNESCO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg Gerson Msigwa amesema tayari wameshaanza kupeleka Maandiko Katika Shirika Elimu Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa ajili ya Kuutambulisha Mziki wa Singeli kama urithi wa Taifa kwa kuwa ni Muziki wenye vionjo na radha za kwetu.
Msigwa amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa mashindano ya CHAN 2024, yanayotarajiwa kuzinduliwa Agosti 02, 2025 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.
Msigwa amesema katika mashindano hayo, mbali na Soka kutakuwa na Tamasha kubwa la muziki wa singeli ambapo pamoja na mambo mengine wanahamasisha kwa kiasi kikubwa muziki huo kwa kuwa umeshika kasi duniani kote hivyo wanataka Dunia Itambue muziki huo asili yake ni Tanzania.
Pia ametoa onyo wa wale ambapo wanatumia sanaa hiyo kuimba hovyo kwani watawashughulikia ili kunusuru Kazi hiyo na kuwataka vijana kuona fursa ya ajira na kuutumia vizuri kwani unalipa.
Kutokana na hayo Wizara imefunga Jukwaa kubwa katika Uwanja wa Taifa ambapo mara ya baada ya mechi ya ufunguzi, Agosti 02, 2025 kati ya Tanzania na Burkina Faso Kumalizika, watu wataendelea kuburudika na muziki huo wa Singeli na hivyo kuwakataka wananchi wajitokeze kwa wingi wakaburudike na Burudani mbalimbali.