Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MAKONDA AKUTANA NA KAMATI YA MAANDALIZI YA AFCON 2027 KUELEKEA HAFLA YA UZINDUZI RASMI WA OFISI ZA CAF


Katika kuelekea mashindano ya AFCON 2027, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amekutana na Kamati ya Ndani ya Maandalizi ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) kwa lengo la kupitia na kuratibu maandalizi ya shughuli mbalimbali kuelekea mashindano hayo.

Kikao hicho ni sehemu ya maandalizi kuelekea uzinduzi rasmi wa makao makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Fainali za AFCON 2027, pamoja na hafla ya utiaji saini mkataba wa ushirikiano kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Katika kikao hicho, Mhe. Makonda amezielekeza kamati zote zinazohusika kuhakikisha zinatimiza majukumu yake kwa weledi na ufanisi, kwa kuzingatia malengo yaliyowekwa ili maandalizi ya AFCON 2027 yafanyike kwa mafanikio.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano miongoni mwa kamati zote, akieleza kuwa AFCON 2027 ni fursa kwa kila Mtanzania kupitia kukuza utalii, uchumi, ajira na kuitangaza Tanzania kimataifa.

slot gacor