Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MREMBO WA DUNIA AWASILI ZANZIBAR


Zanzibar imepokea ugeni wa kipekee katika ulimwengu wa urembo,  Miss World 2026 Joheirry Molla, ambaye amewasili visiwani humo  Novemba 19, 2026 akiambatana na  warembo kutoka mabara sita ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini Tanzania.

Ziara hiyo inalenga kutangaza utajiri wa vivutio vya utalii, utamaduni na uzuri wa Tanzania, huku ikiwa sehemu ya maandalizi na hamasa kuelekea mashindano ya Miss World 2027 yanayotarajiwa kufanyika nchini.

Miss Molla anatarajiwa kutembelea hoteli na maeneo mbalimbali ya utalii yatakayokuwa sehemu ya historia ya mashindano hayo.

Akizungumza mara baada ya kuwasili, Miss Molla amesema amevutiwa na utamaduni wa Tanzania pamoja na mapokezi mazuri aliyopata, akieleza kuwa ana hamu ya kutembelea maeneo mbalimbali ya visiwa hivyo na kujionea uzuri wake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Emmanuel Ishengoma, amesema Serikali inalenga kutumia fursa ya kuandaa mashindano hayo kujinufaisha kiuchumi, kukuza sekta ya utalii, utamaduni na kuitangaza Tanzania kimataifa.

slot gacor