Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MOROGORO KUMENOGA TAMASHA LA UTAMADUNI 2026


Kuelekea Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni mkoani Morogoro kwa mwaka 2026, mkoa huo umeanza shamrashamra kwa matukio ya kukaribisha na kuhamasisha  wananchi kushiriki Tamasha hilo linaloanza Agosti 25 hadi 29 katika Uwanja wa Jamhuri.

Ambapo 24 Agosti, 20226 limefanyika Bonanza la michezo likiwa na jina la Utamaduni Jogging likijumuisha mbio fupi pamoja michezo mbalimbali  ikiwemo riadha, kuvuta kamba, kutembea na mayai kwenye kijiko pamoja na kutembea kwa magunia.

Mgeni rasmi katika tukio hilo akiwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Khalid Matengo ameongoza  bonanza hilo ambalo pia limehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Methusela Ntonda.

Pamoja na washindi wa Bonanza hilo kupewa medali, pia wamehamasishwa kuendelea kushiriki michezo mara kwa mara ili kuimarisha afya zao.

slot gacor