Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

ZABUNI YA UJENZI WA SHULE SABA ZA MICHEZO IMESHATANGAZWA


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Hamis Mwinjuma amesema zabuni ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule za michezo imetangazwa ili kupata mkandarasi.

Kauli hiyo ameisema leo Mei 25,2026 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa  Nkasi Kusini Mh.Moses Ludovicol Kaegele aliyehoji Serikali ina mpango gani wa kujenga shule za michezo kwa kila jimbo hasa katika jimbo la Nkasi Kusini, ili kuibua vipaji vya wanasoka nchini.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Mwijuma, amesema Serikali imedhamiria kujenga shule 56 za michezo katika mikoa yote nchini, ambapo baada ya kukamilika kwa shule hizo kila mkoa unatarajiwa kuwa na shule za michezo angalau mbili.

"Katika kutekeleza mpango huo Serikali imeanza na shule saba za michezo katika mikoa ya Singida,Tanga, Ruvuma, Pwani, Dodoma, Kagera na Mtwara ambapo zabuni ya utekelezaji wa mradi huo tayari imetangazwa, ili kupata mkandarasi wa mradi husika".

Aidha, Katika swali la nyongeza la  Mhe. Ritta Kabati ambaye aliuliza kuwa Kwakuwa michezo ni ajira, afya, Wabunge wamekuwa wakianzisha mashindano ya Michezo mbalimbali katika majimbo, wilaya na mikoa. Je Serikali iko tayari kuwasaidia ili tuweze kuibua vipaji na kuhakikisha kwamba kila Halmashauri inakuwa na viwanja bora vya michezo yote.

Akijibu swali hilo Mhe. Mwinjuma amesema kuwa Serikali inaunga mkono Watu au Taasisi zote binafsi ambazo zimeonesha nia ya kuendeleza michezo katika Sekta mbalimbali wakiwemo Wabunge. Hata hivyo Wizara haijawa na Bajeti ya kutosha ya kuwapa Wabunge ili kuendeleza michezo yao, ila tunaelekea tutaangalia namna ya kuwaunga mkono na kuhakikisha vipaji katika maeneo ya Wabunge vinaendelezwa.

Vilevile kukamilika kwa Shule hizo kutasaidia kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi katika michezo mbalimbali, huku wakipata fursa ya kuendelea na masomo".Amesema Naibu Waziri. 

Pia katika awamu zinazofuata za utekelezaji wa mradi huo, Mkoa wa Rukwa utafikiwa na unatarajiwa kunufaika kwa kuwa na shule mbili za michezo mbalimbali ikiwemo soka.

slot gacor