Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ametembelea Banda la Wizara hiyo, pamoja na mabanda mengine kuona huduma na elimu inayotolewa katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba) leo Julai 8, 2026.