Habari
CRDB BANK GRAND BUNGE BONANZA 2026 LAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Daniel Sillo, ameongoza matembezi ya pamoja katika CRDB Bank Grabd Bunge Bonanza ambalo limelenga kuonesha mshikamano, kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kuhamasisha umuhimu wa michezo kama nyenzo ya kujenga afya, umoja na ushirikiano wa kimataifa.
Bonanza hilo limefanyika leo Juni 20, 2026 jijini Dodoma ambapo limekutanisha Waheshimiwa Wabunge, Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja wadau wa michezo.
Katika bonanza hilo linalofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, timu mbalimbali zinashindana katika michezo tofauti.
