Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

SERIKALI IMEJIPANGA KUTOA HUDUMA AFCON 2027


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027 yanafanyika kwa mafanikio, kwa kuimarisha huduma muhimu zikiwemo malazi, usafiri, usalama na ukarimu kwa wageni na timu zitakazoshiriki.

Waziri Makonda ameyasema hayo jijini Dar es Salaam Novemba 25, 2026 wakati wa uzinduzi wa ofisi itakayoratibu shughuli za mashindano hayo kwa nchi tatu mwenyeji, Tanzania, Kenya na Uganda, ambayo ipo Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Samson Adamu, amesema ushirikiano baina ya nchi hizo tatu ni hatua muhimu katika kuimarisha uratibu na maandalizi ya tukio hilo kubwa la kimataifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema AFCON 2027 itatoa jukwaa muhimu la kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kwa mamilioni ya watu duniani, hatua inayotarajiwa kuongeza hamasa ya utalii na kuvutia wageni wengi zaidi nchini, huku Bodi ya Utalii Tanzania chini ya Mkurugenzi Mkuu wake Dkt. Theresa Mugobi ikiingia makubaliano ya haki za matangazo na wadhamini wakuu wa mashindano hayo.

Michuano ya AFCON 2027 inatarajiwa kuwa jukwaa la kuunganisha mataifa ya Afrika, kukuza utalii, kuongeza fursa za ajira na biashara, pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania, Kenya na Uganda.

Hi ni story hivyo usifupishe bali nipe tafsiri proper kukaa kwenye website

slot gacor