Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MISS WORLD NA MVUTO WA UTAMADUNI WA KIMASAI


Miss World 2026, Joheirry Molla, pamoja na warembo wenzake kutoka mabara sita duniani, wanaendelea na ziara yao nchini Tanzania kwa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii, utamaduni na urithi wa Taifa.

 Novemba 26, 2026, Joheirry Molla anatembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha, ikiwa ni sehemu ya kutambua na kujionea utajiri wa rasilimali za utalii, historia na utamaduni wa Tanzania.

Katika ziara hiyo, warembo hao wanapata fursa ya kufahamu zaidi utamaduni wa Kitanzania, ikiwemo utamaduni wa Kimasai ambao ni miongoni mwa alama zinazotambulisha utambulisho na urithi wa kipekee wa nchi yetu.

Ziara hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kuelekea kuwa mwenyeji wa mashindano ya Miss World mwaka 2027, ambapo nchi inatumia fursa hiyo kutangaza vivutio vyake vya utalii, utamaduni na fursa mbalimbali kimataifa.

Kupitia maandalizi hayo, Tanzania inalenga kutumia jukwaa la Miss World kuongeza mwonekano wake duniani, kuvutia watalii na kuimarisha taswira ya nchi kama kitovu cha utalii, utamaduni na uwekezaji

slot gacor