Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

TANZANIA KUTUMIA AFCON KUTANGAZA UTALII WAKE


Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika Afrika (CAF) wamesaini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati wa kuitangaza Utalii wa Tanzania kama sehemu ya maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika — AFCON PAMOJA 2027.
Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Dkt. Theresa Mugobi, na Katibu Mkuu wa CAF, Samson Adamu, mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa Uzinduzi wa Makao Makuu ya Sekretarieti ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) Uliofanyika Novemba 25, 2026 jijini Dar es Salaam.
Ushirikiano huo unalenga kutumia nguvu ya soka la Afrika kuonesha vivutio vya utalii vya Tanzania, utamaduni wake wa kipekee na ukarimu wa watu wake kwa dunia.
Tanzania, pamoja na Kenya na Uganda, itakuwa mwenyeji wa AFCON PAMOJA 2027, ambapo kupitia fursa hiyo zitaonesha vilivyomo katika ukanda huo achilia mbali soka.

slot gacor