Habari
MHE. KIKWETE ASHUHUDIA HUDUMA ZINAZOTOLEWA B ANDA LA WIZARA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ametembelea Banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kupokelewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw. Gideon Malabeja, kuona huduma na elimu inayotolewa katika banda hilo.
Mhe. Kikwete amefungua Rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika eneo la Chinangali Park, jijini Dodoma leo Juni 17, 2026 .
[6:29 AM, 6/17/2026] Shamimu: Wananchi mbalimbali wanaendelea kutembelea na kupata huduma katika Banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Wiki ya Utumishi wa Umma ianayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma tarehe 17 Juni, 2026.
Banda hilo linaendelea kutoa kuhusu huduma, mafanikio na mipango ya Wizara katika kuendeleza sekta za habari, utamaduni, sanaa na michezo nchini
