Habari
WAZIRI MAKONDA ATETA NA DATAVERA KUHUSU MIFUMO YA KIDIJITALI SEKTA ZA WIZARA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda,
amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Kampuni ya Datavera, ambao ni watalaam wa mifumo ya kidijitali.
Amekutana nao leo Aprili 15, 2026, bungeni, jijini Dodoma, akiwa na wataalam wa wizara, ambapo amepokea wasilisho lao kuhusu mifumo ya kidijitali kwa ajili ya kuimarisha na kuendeleza sekta za wizara.
