Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

BI AISHA DACHI: USHIRIKIANO WA WIZARA NA VYOMBIO VYA HABARI HUSAIDIA KUFIKISHA UJUMBE KWA WANANCHI


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Asha  Dachi,amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Vyombo vya Habari na Wizara katika kuelimisha na kuhabarisha umma kuhusu fursa na maendeleo yanayopatikana katika sekta za wizara.

 Amesema hayo leo Juni 23, 2026 katika Viwanja vya Chiangali Park Dodoma, alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma, ambapo ameshuhudia huduma na elimu inayotolewa kwa wananchi.

Amepongeza juhudi za Wizara katika kusimamia na kuimarisha sekta hizo muhimu, akibainisha kuwa maandalizi yanayoendelea kuelekea Mashindano ya AFCON 2027, yanaonesha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha Tanzania inaandaa mashindano hayo kwa viwango vya kimataifa.

slot gacor