Habari
MISS WORLD, WENZAKE WAZIDI KUVUTIWA NA TANZANIA
Mshindi wa taji la Miss World 2026, Joheirry Molla, akiwa pamoja na warembo sita wa taji la Miss World kutoka mabara mbalimbali, wanaendelea kuvutiwa na uzuri, utamaduni na vivutio vya Tanzania kupitia ziara yao nchini.
Katika ziara hiyo, warembo hao wakiongozana na viongozi wa maandalizi ya Miss World wamefika eneo maarufu la Vijana wa Makachu, Zanzibar, kujionea na kufurahia mchezo wa jadi unaobeba sehemu ya utamaduni na burudani ya Wazanzibari.
Aidha, walimbwende hao wamepata fursa ya kusafiri kwa mashua katika Bahari ya Hindi na kushuhudia mandhari ya kuvutia ya jua likizama (Sunset), tukio lililowapa nafasi ya kufurahia uzuri wa Zanzibar na kumbukumbu za kipekee za ziara yao nchini.
