Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MISS WORLD ATUMA SALAMU ZA KUILINDA BAHARI


Mrembo wa Dunia (Miss World 2026), Joheirry Mola, ametuma ujumbe wa kuhamasisha jamii duniani kulinda bahari, akieleza umuhimu wake katika kuunganisha watu na kuhifadhi urithi wa asili kwa vizazi vijavyo.

Ametoa ujumbe huo akiwa katika Kisiwa cha Nyange, Zanzibar, alipotembelea eneo hilo pamoja na warembo wenzake kutoka mabara sita, ikiwa ni sehemu ya ziara yao nchini Tanzania yenye lengo la kujionea uzuri, utajiri wa vivutio vya utalii, utamaduni na urithi wa Tanzania, kuelekea maandalizi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Miss World 2027.

Joheirry amesema amefurahi kuwa Zanzibar na kupata fursa ya kujifunza na kushiriki katika utamaduni na mila za Kitanzania, huku akiwahimiza watu duniani kutunza bahari.

Amesema bahari ni rasilimali muhimu inayowaunganisha watu, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kuilinda ili kuendelea kuwa na uzuri wake na manufaa kwa maisha ya sasa na vizazi vijavyo.

slot gacor