Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MSIGWA: AFCON 2027 AFE KIPA, AFE BEKI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amesisitiza kuwa, Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2027) ni maelekezo ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, hivyo lazima yafanyike.

Amesema hayo Novemba 11, 2026 Mtumba jijini Dodoma, katika hafla  ya  kuwapongeza Wanamichezo wa wizara hiyo, walioshiriki mashindano ya SHIMIWI mwaka 2026, mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.

Msigwa amesisitiza kuwa, uwepo wa Mashindano ya AFCON mwakani ni moja ya jitihada za Serikali za kuhakikisha Tanzania inajiweka katika ramani ya Dunia kupitia michezo ili kuongeza uchumi na kujitagaza zaidi.

Amewataka viongozi wa wizara hiyo, kila mmoja katika Idara yake kuhakikisha  mashindano hayo yanafanyika kwa mafanikio bila kuweka visingizio vunabyoweza kukwamisha jambo hilo muhimu kwa nchi.

Katika hatua nyingine aliipongeza timu ya wizara iliyoshiriki SHIMIWI 2026 ambapo iliibuka Bingwa wa mchezo wa Draft upande wa Wanawake uliobebwa na Bi. Niuka Chande (Sikitu).

"Nawapongeza kwa kuendelea kufanya vizuri katika michezo, lakini kipekee nampongeza bingwa wetu Sikitu ambaye amekua bingwa wa draft  mara 18 kati ya 20 tokea alipoanza kuingia katika mashindano mwaka 2006, na nitapatia zawadi ya shilingi milioni 3" amesema Msigwa.

slot gacor