Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

AZOA MAKOMBE 18


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa, amewapongeza Wanamichezo wa wizara hiyo waliofanya vizuri katika michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) mwaka 2026 iliyofanyika hivi karibuni mkoani Kilimanjaro.

Ametoa pongezi hizo Novemba 11, 2026 Mtumba jijini Dodoma, katika hafla  ya  kuwapongeza Wanamichezo hao ambapo  wizara iliibuka Bingwa wa mchezo wa Draft upande wa Wanawake uliobebwa na Bi. Niuka Chande (Sikitu).

"Nawapongeza kwa kuendelea kufanya vizuri katika michezo, lakini kipekee nampongeza bingwa wetu Sikitu ambaye amekua bingwa wa draft  mara 18 kati ya 20 tokea alipoanza kuingia katika mashindano mwaka 2006, na nitapatia zawadi ya shilingi milioni 3" amesema Msigwa.

slot gacor