Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MSIGWA ATAKA KASI UJENZI WA UWANJA WA DODOMA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, amemtaka Mkandarasi wa Uwanja wa Dodoma Kampuni ya Limonta kuongeza kasi ya ujenzi wa uwanja huo.

Msigwa ametoa maelekezo hayo Juni 11, 2026 baada ya kushiriki kikao cha kupitia maendeleo ya kazi ya ujenzi (Site Meeting) na kisha kukagua  majengo ya mradi na msingi wa uwanja.

"Changamoto ni sehemu ya kazi na ninataka mkae mzijadili na kuzitatua kama jopo na muhakikishe mnakuwepo wote eneo la kazi muwajibike ipasavyo ili mmalize hii kazi kwa wakati kama tulivyokubaliana" amesisitiza Msigwa.

Mradi huo ambao ulianza Februari, 2025 wenye  uwezo wa kuchukua watu 32,000 umefika asilimia 11 na Mkandarasi anaendelea na ujenzi wa msingi.

slot gacor